Saturday, February 02, 2013

CLINTON: MAREKANI IMEPOTEZA HESHIMA KUISAIDIA ISRAEL


Waziri anayeondoka wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton amekiri kuwa Marekani haina hadhi na nafasi nzuri katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Clinton ambaye alikuwa akizungumza katika kituo cha Baraza la Uhusiano wa Nje wa Marekani katika siku yake ya mwisho kama Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo amesema amekuwa akifuatilia fikra za waliowengi duniani na kwamba anapaswa kukiri kuwa katika muongo mmoja uliopita Marekani haikuwa na hadhi na nafasi nzuri katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. Amesisitiza kuwa sababu ya suala hilo ni uungaji mkono mkubwa wa Marekani kwa utawala wa Israel.
Hillary Clinton pia amesema kuwa siasa za Marekani zimefeli katika ulimwengu wa Kiislamu. Hillary Clinton leo anakabidhi mikoba ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa John Kerry baada ya kuhudumu katika wizara hiyo tangu mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO