Sunday, February 03, 2013

IRAN INA HAKI YA KUTUMIA NYUKLIA


Serikali ya China imesisitiza kwamba, Iran ina haki kamili ya kunufaika na teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Hong Lei, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China amesema kuwa, daima Beijing imekuwa ikiunga mkono ushirikiano wa Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Amesema, China inaamini kwamba, mazungumzo na ushirikiano ndio njia pekee na sahihi ya kuondoa suutafahumu kuhusiana na suala la miradi ya nyuklia ya Iran na imekuwa ikizishajiisha pande mbili hizo kushirikiana zaidi. Msemaji huyo wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China ameongeza kuwa, Iran ikiwa miongoni mwa nchi zilizotia saini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia NPT ina haki ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Licha ya kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ni kwa ajili ya matumini ya amani na imekuwa ikifanyika chini ya usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, lakini Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wao wamekuwa wakiituhumu Tehran kwamba, miradi yake ya nyuklia ni kwa ajili ya malengo ya kijeshi, tuhuma ambazo hazina msingi wowote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO