Sunday, February 03, 2013

JESHI LA IRAN LAZINDUA KIFARU KIPYA


Katika siku ya tano ya maadhimisho ya 'Alfajiri 10 za Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu' Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litazindua kizazi kipya cha vifaru viwili aina ya Zolfaqar na Samsam. Uzinduzi huo utafanyika katika Jumatatu Februari 4 katika Kituo cha Utafiti na Jihadi ya Kujitosheleza ya vikosi vya nchi kavu vya Jeshi la Iran.
Aina hii mpya ya vifaru imebuniwa na kutengenezwa kikamilifu na wataalamu wa Iran. Hii ni katika hali ambayo hapo jana pia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizindua ndege ya kivita yenye umbo pekee duniani iliyotengenezwa hapa nchini. Ndege hiyo iliyopewa jina la Qaher 313 ina uwezo wake ni sawa na ndege ya kivita ya Marekani ya F/A 18.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO