Monday, February 04, 2013

KOREA KUSINI YAITAHADHARISHA KASKAZINI KUHUSU NYUKLIA


Korea Kusini imetahadharisha kwamba hatua ya Korea Kaskazini ya kutaka kufanya duru ya tatu ya jaribio la nyuklia itakuwa tishio kubwa kwa eneo hilo.

Waziri wa Masuala ya Kigeni ya Korea Kusini Yu Woo-ik amesema, Korea Kaskazini inaazimia kufanya jaribio jingine la nyuklia, lakini haijatoa maelezo ya kuridhisha juu ya suala hilo. Ameongeza kuwa, iwapo hatua za mwisho za jaribio hilo zitakamilishwa kwa mafanikio, suala hilo litamaanisha kuwa usalama wa Peninsula ya Korea uko hatarini zaidi.
Naye Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo ameeleza wasiwasi wake juu ya jaribio hilo na kutahadharisha kwamba, iwapo Pyongyang itafanya jaribio hilo hatua hiyo itakuwa ni sawa na kuchokoza jamii ya kimataifa kwani ni tishio kubwa kwa Seoul.
Marekani, Korea Kusini na nchi nyinginezo zimeitaka Korea Kaskazini isifanye majaribio ya nyuklia la sivyo itakabiliwa na hatua kali. Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya nyuklia mwaka 2006 na mwaka 2009 na kuwekewa vikwazo mbalimbali kimataifa

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO