Monday, February 04, 2013

KIONGOZI NAMBARI 3 WA MALI AKAMATWA


Kiongozi nambari 3 wa kundi la waasi wa Answaruddin la kaskazini mwa Mali amekamatwa karibu na mpaka wa Algeria alipokuwa akikimbia mashambulizi ya vikosi vya jeshi la Ufaransa.

Muhammad Moussa amepelekwa katika mji wa Kidal uliokuwa ngome ya mwisho ya waasi wa Mali, walikofurushwa katika mashambulizi ya vikosi vya nchi hiyo vikisaidiwa na askari wa Ufaransa. Taarifa za kukamatwa kiongozi huyo wa waasi zimethibitishwa na Abdoulaye Toure, afisa wa serikali ya Mali katika eneo la Kidal aliyesema kuwa, kiongozi huyo wa waasi amekamatwa na kundi jingine hasimu la waasi wa kaskazini mwa Mali la Tuareg.  
Wakati hayo yakiripotiwa ndege za vita za Ufaransa zimeendelea kushambulia kambi za waasi karibu na mji wa kaskazini mwa Mali wa Tessalit, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Algeria. Thierry Burkhard msemaji wa jeshi la Ufaransa amesema, mashambulizi hayo yalianza jana usiku na yamelenga maeneo muhimu na kambi za mafunzo zilizoripotiwa kutumiwa na wapiganaji wa kundi la al Qaida.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO