Monday, February 04, 2013

MELI YA MAFUTA YA UFARANSA YATEKWA NYARA


Maafisa wa bandari ya Abidjan nchini Cote d'Ivoire wamethibitisha kuwa meli ya mafuta ya Ufaransa imetekwa na maharamia karibu na pwani ya nchini hiyo. Afisamawasiliano wa bandari hiyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba meli hiyo imetekwa ikiwa katika eneo la kimataifa baharini.
Shirika la kimataifa la usafiri wa majini lilikuwa limeripoti kupotea kwa meli hiyo mwishoni mwa juma lililopita. Serikali ya Ufaransa ilisema kuwa meli hiyo inayopeperusha bendera la Luxembourg ilikwa na mabaharia 19 kutoka Togo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO