Monday, February 04, 2013

ISRAEL YAKAMATA WAPALESTINA 23


Israel imewakamata wanachama 23 wa Hamas katika eneo la Ukingo wa Magharibi inalolikalia. Miongoni mwa waliokamatwa ni wabunge wa chama hicho. Kukamatwa kwao kumethibitishwa na Hamas na pia Israel.
Tangazo la Hamas limesema kuwa wabunge watatu wa chama hicho walikamatwa alfajiri ya leo, pamoja na viongozi wengine wa Hamas katika eneo hilo. Hamas imesema kitendo hicho ni uhalifu ambao hautasimamisha mapambano. Msemaji wa serikali ya Israel amekataa kuthibitisha kukamatwa kwa wabunge hao, lakini alisema kuwa wapalestina 25 wamekamatwa, 23 miongoni mwao wakiwa wanachama wa Hamas.
Chama cha Hamas ambayo huchukuliwa na Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya kama kundi la kigaidi, kilishinda uchaguzi wa wapalestina mwaka 2006. Mwaka 2007 serikali ya mseto kati yake na chama cha Fatah ilivunjika, na Hamas ikauteka ukanda wa Gaza kutoka mamlaka ya wapalestina inayoongozwa na chama cha Fatah.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO