Friday, March 01, 2013

MRIPUKO WAUA WATU WAWILI PALESTINA

Mripuko uliotokea leo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, umepelekea watu wawili kuuawa. Polisi ya utawala haramu wa Kizayuni imetangaza kutokea mripuko huo mapema leo katika mji wa Rishun Litsun ulioko karibu na mji mkuu wa Israel Tel Aviv na kwamba, watu wawili wameuawa. Kanali ya 10 ya teevisheni ya utawala huo imetangaza kuwa, mripuko huo umetokea majira ya asubuhi na kwamba, mbali na kuuawa watu wawili, umesababisha hasara kubwa ya mali. Katika siku za hivi karibuni miji tofauti ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, imekuwa ikishuhudia vitendo vya ukatili na miripuko ambayo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, vinasababishwa na mamafia wanaojihusisha na biashara za madawa ya kulevya na wanaoupinga utawala wa Kizayuni wa Israel. Hii ni katika hali ambayo, tangu awali utawala wa Kizayuni umekuwa ukiwataka Mayahudi duniani kwenda kuishi huko katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu kwa kisingizio kwamba, ni ardhi za peponi walizoahidiwa, huku hali ya mambo ikionyesha kinyume chake.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO