Saturday, March 02, 2013

NCHI ZAIDI YA MIA ZAUNGA MKONO NYUKLIA YA IRAN

Mwakilishi wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema kuwa nchi zaidi ya 100 wanachama wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande wowote (NAM) kwa mara nyingine tena zimeunga mkono miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani. Ali Asghar Sultaniye amesema kuwa masuala mbalimbali ikiwemo taarifa kuhusu uungaji mkono wa harakati ya NAM kwa miradi ya nyuklia ya Tehran yenye malengo ya amani yamejadiliwa na kupasishwa katika kikao cha jana cha wawakilishi wa NAM katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA. Ali Asghar Sultaniye Mwakilishi wa Iran katika wakala wa IAEA amesistiza kuwa  taarifa hiyo iliyo na ujumbe chanya unaeleza kuwa nchi zaidi ya 100 duniani zinaunga mkono shughuli za nyuklia za Iran zenye malengo ya amani kwa mujibu wa mkataba unaopiga marufuku uundaji na uenezaji wa silaha za nyuklia NPT na kwa mujibu wa hati ya wakala wa IAEA. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO