Rais mpya wa China Xi Jinping amewasili leo nchini Urusi kwa ziara yake ya  kwanza  ya nchi za kigeni tangu kuapishwa kuwa rais mapema mwezi huu. Xi  na Rais wa Urusi Vladimir Putin wanatarajiwa kutia saini makubaliano kadhaa  hasa ya masuala ya nishati na uwekezaji ukiwemo mkataba utakaopelekea  Urusi kuongeza kiwango cha mafuta inachouza kwa China. Xi atazuru mataifa  manne yakiwemo Tanzania, Congo Brazzaville na Afrika kusini anakotarajiwa  kuhudhuria mkutano wa BRICS unaoleta pamoja mataifa ya  Brazil,Urusi,India,China na Afrika kusini. 

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO