Saturday, April 13, 2013

MALI ZA BIN ALLY ZAKABIDHIWA KWA TUNISIA

Lebanon imeirejeshea Tunisia dola za Kimarekani zisizopungua milioni 29 zilizokuwa katika benki moja ya Lebanon mali ya familia ya Zainul Abidin bin Ali wa Tunisia aliyepinduliwa madarakani. Cheki hiyo ya thamani ya dola za Kimarekani milioni 28.8 ambayo imekuwa kwenye akaunti ya benki moja ya Lebanon mali ya Laila Trabelsi mke wa bin Ali imekabidhiwa kwa Rais Munsif Marzouk wa Tunisia na Ali bin Fetas al Marri Mkuu wa Timu ya Umoja wa Mataifa Inayofuatilia Mali Zilizoibiwa. Marri aliteuliwa na Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka jana kuwa Wakili Maalumu wa umoja huo anayesimamia urejeshaji wa mali na fedha zilizoibiwa na viongozi wa nchi waliopinduliwa madarakani katika mapinduzi ya wananchi  katika eneo la kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO