Saturday, March 02, 2013

ZEIDAN ASEMA HAKUNA MAJESHI YA KIGENI


Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan amesema nchi yake inapinga vikali ujenzi wa kambi za majeshi ya nchi za kigeni katika ardhi ya Libya. Zeidan ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Tripoli amesema serikali yake haijatoa ahadi kwa nchi yoyote ya kujenga kambi za majeshi ya kigeni nchini humo. Ameongeza kuwa Libya haitakubali ujenzi wa kambi za majeshi ya kigeni katika ardhi yake na kwamba madai yanayoenezwa kuhusu suala hilo hayana msingi wowote.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Libya amesema kuwa serikali yake imeazimia kupambana na makundi ya wanamgambo yanayopora mali za wananchi. Baadhi ya makundi ya wanamgambo walioshiriki katika kuangusha utawala wa dikteta wa zamani wa Libya yamekuwa yakilaumiwa kwa kujihusisha na harakati zinazovuruga usalama na amani nchini Libya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO