Tuesday, April 23, 2013

ARAB LEAGUE YAKAIDI AGIZO LA BAN KI MOON


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu 'Arab League' amepuuza takwa la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kusimamishwa upelekwaji wa misaada ya kijeshi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa makundi ya waasi na ya kigaidi nchini Syria.
Nabil al Arabi amesisitiza kuwa, hakuna kitu chochote kitakachoweza kuzuia uungaji mkono wa jumuiya hiyo kwa waasi wanaopambana na serikali ya Syria. Ameongeza, kwa sasa hakuna matumaini ya kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za kisiasa.
Hivi karibuni Valerie Amos, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya misaada ya kibinadamu aliliambia Baraza la Usalama kwamba, mauaji yanayofanywa na makundi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio na hatia nchini Syria, kubomolewa majumba na hata vitendo vya  magaidi hao vya kuwatesa  wanawake na watoto vimeshadidisha zaidi mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO