Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DDP)
kulitaka Jeshi la Polisi kumwachia mtuhumiwa Mussa Omar Makame kutokana na
ushahidi kutojitosheleza, jeshi hilo sasa limeingia kwenye mkorogano. Wiki iliyopita jeshi hilo lilitangaza kumkamata Makame pamoja na watuhumiwa
wengine na kudai kuwa ndiye aliyemuua Paroko wa Parokia ya Mpendae, Padri
Evarist Mushi, kwa risasi huku wenzake wakitajwa kuhusika kuwajeruhi viongozi
wengine wa dini. Tukio hilo pia liligusiwa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya mwisho
wa mwezi Machi, akisema limehusisha vyombo vya nje vikishirikiana na jeshi la
polisi nchini. Hata hivyo, jeshi hilo jana lilikana kushirikiana na vyombo vya nje katika
uchunguzi huo uliomtia hatiani Makame baada ya ushahidi wao kukataliwa na
Mkurugenzi wa Mashataka, Ibrahimu Mzee Ibrahimu.
Katika mahojiano na gazeti hili, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa A. Mussa,
alikanusha jeshi la polisi kushirikiana na kikosi cha upelelezi cha Marekani
(FBI) ili kumkamata Makame. Kauli yake inakinzana na ile aliyoitoa Machi 23, mwaka huu aliposema
uchunguzi huo ulikuwa ukifanywa na makachero wa polisi kwa kushirikiana na
wapelelezi kutoka Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kufanikisha
kumkamata mtuhumiwa huyo. Hatua hiyo ilikuwa ni baada ya jeshi hilo kulaumiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo
Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polikarp Kardinali Pengo, kuwa limekuwa
kimya kuhusu matukio hayo na kusingizia kwamba yanafanywa na vikundi vya
wahuni........................
endelea
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO