Ripoti mpya zimeibuka mwishoni mwa juma lililopita juu ya vitendo vya kijasusi vya Marekani duniani, wakati huu ambapo Mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Kijasusi Edward Snowden bado akiripotiwa kuwa katika uwanja wa Ndege wa Urusi akiwa katika harakati za kutafuta hifadhi. Snowden bado yu jijini Moscow kwa siku ya 16 hii leo.hapo jana alijitokeza tena mbele ya vyombo vya Habari akishutumu kuwa Shirika la usalama wa Taifa la Marekani (NSA) linashirikiana na nchi nyingine za Magharibi kuingilia mamilioni ya mawasiliano ya simu na Barua pepe nchini Brazili. Snowden amesema kuwa Shirika hilo linashirikiana na mashirika mengine ya kigeni kwa siri.
Gazeti la kila siku nchini Brazili O Globo, limeripoti kuwa kwa mujibu wa Snowdea, NSA limefanya vitendo vya kijasusi dhidi ya Wakazi na Kampuni pia Watu wanaosafiri nchini Brazili. Taarifa zinasema kuwa idadi kamili ya Watu haijulikani, lakini Mwezi Januari mwaka jana, Brazili ilikuwa ya pili ikiifuata Marekani, ambapo mawasiliano ya simu bilioni 2.3 na ujumbe wa simu ulikaguliwa. O Globo limesema kuwa Mradi huo ulipewa jina la FAIR VIEW ambao NSA ilishirikiana na Kampuni kubwa ya simu nchini Marekani ili kuweza kupata Taarifa za mitandao ya makampuni mengine ya nchi za Ng'ambo zenye ushirika na kampuni ya simu ya Marekani.
Taarifa hizi zimeigusa Serikali ya Brazili kwa kiasi kikubwa ikisema kua tuhuma hizi ni nzito, msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Brazil Tovar Nunes ameeleza.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO