Sunday, April 14, 2013

KERRY KUPANGA MIKAKATI NA CHINA JUU YA KOREA

Waziriwa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasili nchini China kuzungumza na serikali ya china na kuitaka Beijing kutumia ushawishi wake kuizidi nguvu Korea Kaskazini. Kabla ya ziara yake, Waziri Kerry alisema kwamba sera ya kupinga mpango wa nyuklia inayoungwa mkono na marekani na China inapaswa kuwa na meno yenye makali.

Ziara ya siku nne ya Waziri Kerry barani Asia inakuja huku kukiwa na uvumi kwamba Korea Kaskazini inafanya maandalizi kwa ajili ya kuanza mashambulizi ya kombora. Hata hivyo Marekani imesema hakuna ushahidi kuwa Korea ya Kaskazini inaweza kushambulia kwa silaha za makombora ya nyuklia, taarifa ambayo inapishana na ripoti iliyovuja awali ikidai korea kaskazini tayari imetegesha makombora mawili katika pwani yake ya upande wa mashariki.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO