Upinzani nchini Lebanon unaoungwa mkono na Saudi Arabia na nchi za magharibi, umejiimarisha katika kinyang'ayiro cha kumpata Waziri mkuu, baada ya mwanasiasa maarufu Walid Jumblatt kumuunga mkono mgombea aliyeteuliwa kuwania wadhifa huo na kuchukua nafasi liyoachwa na mtangulizi wake aliyekuwa akiungwa mkono na chama cha Hezbollah .
Upinzani unaojulikana kama "Muungano wa Machi 14," umemteuwa Tammam Salam kuwa mgombea wake kuchukua nafasi ya waziri mkuu Najib Mikati aliyejiuzulu mwezi mmoja uliopita. Kuungwa mkono kwa Salam na chama cha Jumblatt cha Progressive Socialist cha jamii ya Wadruze, kinampa mgombea huyo uungaji mkono wa wabunge 67 kati ya 128. Salam, mwenye umri wa miaka 67, anaonekana kuwa ni mtu mwenye msimamo wa wastani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO