Monday, April 29, 2013

SAYYED HASHEM: TUKO TAYARI KWA NJAMA ZA WAZAYUNI

Mkuu wa Baraza la Utendaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hashem Safieddine amesema kuwa, Hizbullah imejiandaa kikamilifu dhidi ya njama na mipango ya uharibifu ya Marekani, Magharibi na Wazayuni. Sayyed Hashem Safieddine amesisitiza kuwa, kile kinachofanywa na Marekani huko nchini Syria si kingine ghairi ya uharibifu na kujaribu kuigawa nchi hiyo na kwamba, njama hizo hazitaishia katika mipaka ya Syria bali zitaenea katika nchi mbalimbali za eneo zikiwemo Iraq, Misri, Lebanon na Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Ameongeza kuwa, hivi sasa njama kubwa zinazofanywa na Marekani na Magharibi ni kuwasha moto wa mapigano ambao utaziteketeza nchi za eneo na kwamba, kama ilivyo ada Harakati ya Mapambano ya Hizbullah haitaacha kukabiliana na njama hizo kwa kutumia silaha yake iliyo huru na ambayo ilipata nguvu baada ya vita vya siku 33 na adui Mzayuni. Aidha ameashiria vitisho vya Wazayuni dhidi ya Lebanon vinavyotokana na madai ya kutungua ndege isiyo na rubani inayodaiwa kumilikiwa na harakati ya Hizbullah ya Lebanon karibu na bandari ya kaskazini mwa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, na kuongeza kuwa, Israel inafahamu vizuri kuwa, vitisho vyake hivyo havina taathira yoyote kwani muqawama umejiandaa vilivyo kujibu hujuma yoyote ile.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO