Monday, April 29, 2013

WAZIRI MKUU WA SYRIA AKOSWA NA BOMU

Habari kutoka Damascus nchini Syria zinasema kuwa msafara wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Wael al-Halki umeshambuliwa mapema leo lakini kiongozi huyo hakujeruhiwa. Habari zaidi zinasema kuwa shambulio hilo la bomu limesababisha kifo cha mlinzi mmoja wa Waziri Mkuu huyo. Kanali ya al-Akhbariyah imeonyesha video baada ya shambulio hilo katika eneo la Mezze ambapo majumba kadhaa yamevunjika madirisha kutokana na uzito wa milipuko hiyo. Rais Bashar Asad amelaani shambulio hilo na kuapa kuendeleza mapambana dhidi ya magaidi wanaojaribu kuvuruga nchi kwa msaada wa Wamagharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu. Wael al-Halki baadaye ameonekana akiongoza mkutano wa wanauchumi ofisini kwake akiwa mzima wa afya

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO