Tuesday, April 23, 2013

UBALOZI WA UFARANSA WALIPIUWA NCHINI LIBYA

Ufaransa imelaani shambulio la bomu la kutegwa kwenye gari lililotokea leo kwenye ubalozi wake nchini Libya. Shambulio hilo lililotokea kwenye mji mkuu wa Tripoli, limewajeruhi walinzi wawili. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amesema Ufaransa kwa kushirikiana na viongozi wa Libya watahakikisha wanawabaini haraka wahusika wa shambulio hilo. Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya, Mohammed Abdel Aziz, ameliita shambulio hilo kama kitendo cha kigaidi. Amesema Libya inalaani kitendo hicho dhidi ya taifa lililoisaidia Libya wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Muammar Gaddafi. Wapiganaji wamekuwa wakiwalenga wanadiplomasia, ambapo Septemba mwaka uliopita balozi wa Marekani na Wamarekani wengine watatu waliuawa katika shambulio kwenye ubalozi mdogo mjini Benghazi. Wakati huo huo, Fabius leo anaelekea mjini Tripoli, kutokana na shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO