Bunge la Ugiriki limepitisha hatua zaidi ya kubana matumizi, ikiwemo  kupunguza nafasi 15,000 za ajira ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao wa  2014. Sheria hiyo pia imerefusha kodi ya mali kwa mwaka mmoja mwingine.  Baada ya mjadala wa siku moja, serikali ya Ugiriki imepitisha sheria yenye  kurasa 110 katika kifungu kimoja. Wakopeshaji wa kimataifa wa Ugiriki  wanaitaka nchi hiyo ipunguze gharama zake kabla haijapatiwa msaada wa  Euro bilioni 8.8 kwa ajili ya kuuokoa uchumi wake. Hata hivyo, wananchi wa  Ugiriki wameingia mitaani kwenye mji mkuu wa Athens, kupinga hatua hiyo ya  serikali ambayo ni ndogo kuliko ilivyotarajiwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO