Rais Hamid Karzai wa Afghanistan ametahadharisha juu ya uingiliaji wowote wa 
kigeni katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Amesema wananchi wenyewe ndio 
wanaoapasa kuongoza mchakato wa uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Rais Hamid 
Karzai aliyasema hayo jana katika mkutano wa baraza la usalama la serikali ya 
Afghanistan huko Kabul. Katika mkutano huo maafisa wa ngazi ya juu wa 
Afghanistan pia waliahidi kuwa uchaguzi ujao wa rais utakuwa huru na wa 
kiadilifu. Itakumbukwa kuwa Rais Hamid Karzai mwaka jana alisema kuwa kuweko 
wageni katika tume ya kusimamia uchaguzi ya Afghanistan ni dhidi ya kujitawala 
nchi hiyo. Uchaguzi wa rais wa Afghanistan umepangwa kufanyika Aprili 5 mwaka 
2014.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO