Serikali ya Pakistan leo imekataa kumfungulia mashtaka ya uhaini, kiongozi  wa zamani wa kijeshi wa nchi hiypo, Pervez Musharraf, na imeiambia  Mahakama Kuu kwamba hiyo ni zaidi ya mamlaka yake. Hatua hiyo angalau  itampa nafuu kidogo, Musharraf ambaye tayari yuko katika kizuizi cha  nyumbani kutokana na shtaka moja kati ya matatu yanayomkabili, anayodaiwa  kuyafanya akiwa madarakani kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2008. Kesi  hizo zinasikilizwa katika mahakama za mwanzo. Musharraf amekuwa  akitishiwa kuuawa na kundi la Taliban na amezuiwa kushiriki katika uchaguzi  mkuu ujao. Mahakama Kuu inasikiliza ombi la mawakili wanaotaka Musharraf  afunguliwe mashtaka ya uhaini kwa kukiuka katiba. Nchini Pakistan, ni serikali  pekee inayoweza kumfungulia mtu kesi ya uhaini, ambayo adhabu yake ni  hukumu ya kifo.

No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO