Sunday, April 28, 2013

WAASI NA SERIKALI YA SUDAN WASHINDWA KUAFIKIANA


Duru ya kwanza ya mazungumzo ya moja kwa moja ya amani baina ya serikali ya Sudan na waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini imemalizika bila ya kuwa na natija. Taarifa zaidi zinasema kuwa, duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja baina ya serikali ya Khartoum na Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini ilifanyika jana kwa usimamizi wa Thabo Mbeki mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa na kumalizika bila natija yoyote. Kila upande miongoni mwa pande mbili hizo umeutuhumu upande wa pili kuwa ndio chanzo cha kushindwa mazungumzo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mazungumzo hayo, Thabo Mbeki mpatanishi wa Umoja wa Afrika katika mazungumzo ya amani ya Sudan amesema kwamba, Khartoum na Harakati ya Ukombozi wa Sudan tawi la kaskazini wameshindwa kufikia mwafaka kuhusiana na ratiba ya mazungumzo yajayo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO