Friday, May 24, 2013

17 WAUAWA KWA SHAMBULIZI LA MUHANGA NIGER


Waziri wa ulinzi wa Niger amesema kuwa takriban wanajeshi 17 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mashambulio mawili tofauti kaskazini mwa nchi. Mashambulio hayo yametekelezwa na washambuliaji wa kujitolea mhanga. Mashambulio hayo mawili yalitekelezwa wakati watu wakijiandaa kwa maombi ya asubuhi kabla ya saa tano. Kulingana na waziri wa ulinzi Mahamadou Karidjo Washambuliaji waliendesha gari lililokuwa na vilipuzi katika kambi ya kijeshi ya Agadez na kusababisha mauaji ya watu 17. Zaidi ya watu 20 walijeruhiwa wakiwemo raia. Washambuliaji wanne wameripotiwa kuuawa na polisi wanachunguza eneo la tukio na pia maeneo ya mji ambapo wanaamini kunaweza kuwa na washambuliaji zaidi.
Shambulio la pili lilitokea katika kiwanda cha madini ya uranium cha Arlit, ambacho huendeshwa na kampuni ya ufaransa ya Areva. Maafisa wa kampuni hiyo wanasema Takriban watu 13 walijeruhiwa. Waziri wa ulinzi ameiambia BBC kuwa makundi ya wapiganaji yenye uhusiano wa karibu na al-Qaeda yanahusika katika mashambiulio hayo. Mmoja wa washambuliaji hao, aliendesha gari lake liliokuwa na bomu na kupita katika kizuizi cha polisi, mjini Agadez kabla asubuhi leo.
Alilipua bomu na kujiua mwenyewe katika shambulizi hilo huku akiwajeruhi wanajeshi watatu kutoka Niger.
Wakati huohuo, gari lengine lililokuwa na bomu lilipuka katika kampuni ya madini ya uranium ambayo inamilikiwa na kampuni ya kifaransa Areva mjini Arlit. Mshambuliaji alifariki na kampuni inasema kuwa wafanyakazi wake kumi na watatu wamejeruhiwa. Wanajeshi wa Niger kinasaidiana na kikosi cha jeshi la Ufaransa kinachokabiliana na wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO