Monday, May 13, 2013

HALI YA AMANI KATI YA CHINA NA JAPAN TETE


Meli za kivita za China zimewasili katika maji ya karibu na visiwa vinavyogambaniwa kati ya nchi hiyo na Japan. Shirika la habari la Kyodo limeriporti kuwa meli mbili za upelelezi za China zimeingia katika maji ya pwani mwa nchi hiyo na karibu na visiwa vinavyozozaniwa na pande hizo mbili katika bahari ya China Mashariki.
Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Asia na Pacific katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan Shinsuke Sugiyama amesema kuwa, Tokyo imewasilisha malalamiko yake ka viongozi wa China.
Ni kwa mara kadhaa sasa ambapo meli za kivita za China zimeingia katika maji ya eneo hilo tangu mwaka 2012 na baada ya serikali ya Japan kununua visiwa hivyo.
Beijing na Tokyo zinahitilafiana juu ya umiliki wa visiwa hivyo vilivyoko katika Bahari ya China Mashariki ambavyo Japan inaviita kwa jina la Senkaku na China inaviita Diayu.
Japan ilivinunua visiwa hivyo kutoka kwa watu binafsi, suala ambalo liliikasirisha mno serikali ya China.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO