Sunday, May 12, 2013

ISRAEL YAISHAMBULIA DRONE YAKE NYINGINE

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeitungua ndege yake isiyo na rubani (drone) aina ya Shoval juu ya bahari ya Mediterranean kwa madai ya matatizo ya kiufundi. Mtandao wa Intaneti wa Ynetnews wa utawala wa Kizayuni umeripoti kuwa ndege hiyo isiyo na rubani ya Israel imetunguliwa na jeshi la utawala huo ikiwa katika operesheni zake za kawaida juu ya bahari ya Mediterranean kutokana na kupata matatizo ya kiufundi jana Jumamosi.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, helikopta za Israel zimeruka juu ya usawa wa bahari katika eneo la baina ya Tel Aviv na Netanya kujaribu kutafuta mabaki na ndege hiyo. Israel imeacha kabisa kutumia ndege zake zisizo na rubani aina ya Shoval ambazo inadaiwa kuwa ni moja ya ndege zake za kisasa kabisa ili kufanya uchunguzi juu ya sababu zinazopelekea ndege hizo zipate matatizo ya mara kwa mara ya kiufundi.
Mwaka jana pia ndege ya Israel isiyo na rubani aina ya Eitan ilianguka kwenye eneo la Moshav Yesodot, katikati ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni kutokana na makosa ya kibinaadamu na ya kiufundi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO