Wednesday, May 15, 2013

URUSI NA ISRAEL ZAKUTANA KUIJADILI SYRIA

Rais wa Urusi Vladmir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekutana kujadili mgogoro unaondelea nchini Syria. Katika mkutano wao uliyofanyika katika makaazi ya kiongzi huyo wa Urusi yaliyoko Sochi, wawili hao walikubaliana kuwa juhudi za kimataifa zinahitajika kumaliza mgogoro wa Syria na kuuzuwia kusambaa katika mataifa ya jirani. Ni taarifa kidogo tu zilizotolewa kuhusu mkutano huo wa siri, lakini wadadisi wanaamini Israel iliutumia kuionya Moscow dhidi ya mpango wake wa kutuma silaha nchini Syria. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, naye anatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Urusi wiki hii kwa mazungumzo na rais Putin. Urusi ni mshirika muhimu wa rais Bashar al-Assad na mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO