Saturday, June 22, 2013

HAMAS YAWANYONGA MAJASUSI WAWILI

Viongozi wa kundi la Hamas wamesema wamewanyonga Wapalestina wawili waliopatikana na hatia ya kupeleleza kwa niaba ya Israel yapata muongo mmoja uliopita na kuwafanya watu wa kwanza kunyongwa tangu kumalizika kwa mwezi mmoja wa msamaha uliotolewa kwa wanaotoa taarifa za kijasusi mwezi April.Wapalestina 16 wamenyongwa mjini Gaza kwa madai hayo ya upelelezi tangu Hamas inyakue eneo hilo mwaka 2007.Kundi hilo la Hamas ambalo haitambui Israel kama taifa halali, imesema kunyongwa kwa watu hao kunalenga kuwazuia Wapalestina kutoka Gaza, kutoa taariifa kwa Israel kama vile kuhusu mahala waliko viongozi wa wanamgambo hao na maghala ya silaha.Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanasema kunyongwa huko kunakiuka sheria za Mamlaka ya Wapalestina ambayo inasema kuwa kesi za aina hiyo zinapaswa kuidhinishwa na Rais Mahmoud Abbas lakini Hamas haitambui utawala wa Abbas.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO