Tuesday, June 11, 2013

LEBANON YAKOSOA UMOJA WA NCHI ZA KIARABU

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Lebanon amekosoa vikali misimamo isiyo wazi ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusiana na mgogoro wa Syria. Adnan Mansour amesema kuwa, tokea ulipoanza mgogoro wa Syria Jumuiya Nchi za Kiarabu haijawahi kuchukua uamuzi wowote ulio wazi kuhusiana na nchi hiyo. Waziri huyo amekadhibisha vikali tuhuma zilizoelekezwa dhidi ya muqawama wa Lebanon na kuongeza kuwa, kuna ulazima wa kufanyika mabadiliko ya kimlingano katika eneo, kwani bila ya Syria hakuna amani itakayopatikana katika eneo kutokana na  nchi hiyo kusimama kidete dhidi ya siasa za kutaka kujitanua za utawala wa Kizayuni wa Israel. Adnan Mansour amesema kuwa, kile kinachojiri nchini Syria ni utangulizi wa kuliweka  eneo hilo chini ya udhibiti wa utawala wa Israel na kukomeshwa kadhia ya Palestina na muqawama wa Lebanon. Ameongeza kuwa, mgogoro wa Syria ni mkubwa mno kwani magaidi kutoka zaidi ya nchi 40 wamejitumbukiza kwenye mgogoro huo na kutenda mauaji na jinai kubwa dhidi ya binadamu nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO