Saturday, June 01, 2013

MAFURIKO YAIKUMBA OKLAHOMA BAADA YA KIMBUNGA

Mafuriko yamekumba mji wa  Oklahoma nchini Marekani muda mfupi baada ya mji huo kukumbwa na vimbunga ambavyo vimewaua watu watano akiwemo mwanamke mmoja na mwanawe.Maeneo mengi ya mji wa Oklahoma yamefurika maji huku mvua kubwa ikisababisha mafuriko ya kima cha urefu wa sentimita 25.Shughuli za usafiri zimetatizika huku uwanja wa ndege wa Will Rogers ukiwahamisha wasafiri hadi maeneo salama  na shirika la gesi na umeme mjini humo likisema kuwa zaidi ya watu 50,000 wameachwa bila umeme.Shirika la utabiri wa hali ya hewa lilitoa hapo jana ilani ya tahadhari ya kuweko kwa hali mbaya ya hewa inayoambatana na vimbunga na mafuriko.Hali hiyo inawadia siku 11 tu baada ya kimbunga kibaya zaidi kukumba mji wa Moore na kusababisha vifo vya watu 24,kumi  kati yao wakiwa watoto.Kimbunga kingine kikali kimekumba jimbo  la Missouri hii leo huku vimbunga vyengine vikielekea majimbo ya mashariki.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO