Saturday, June 01, 2013

MMAREKANI AUAWA KATIKA MAPAMBANO NCHINI SYRIA

Jeshi la Syria limemuua mwanamke Mmarekani na raia wengine wawili wa Uingereza ambao walikuwa katika kundi la kigaidi linalopata himaya ya kigeni katika mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Televisheni ya kitaifa ya Syria imemtaja Mmarekani huyo kuwa ni Bi. Nicole Lynn Mansfield ambaye akiwa na wenzake wawili walikuwa wanachama wa kundi la kigaidi linalojiita Jabhat al-Nusra ambalo lina mfungamano na mtandao wa al-Qaeda. Wanajeshi wa Syria waliwavizia magaidi hao wa kigeni walipokuwa kwenye gari huko Idlib. Wamepatika wakiwa na idadi kubwa ya silaha, kompyuta, ramani za idara muhimu za serikali na bendera ya kundi la kigaidi la al-Nusra.
Syria imekumbwa na machafuko kuanzia Machi 2011 ambapo idadi kubwa ya watu wasio na hatia na maafisa wa usalama wameuawa. Serikali ya Syria inasema machafuko hayo yanachochewa kutoka nje ya nchi na kwamba idadi kubwa ya magaidi ni raia wa kigeni. Serikali ya Syria inazilaumu nchi za Maghairbi na waitifaki wao katika eneo hasa Israel, Qatar, Saudi Arabia na Uturuki kuwa ndio waungaji mkono wakuu wa mgaidi wanaotaka kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar al Assad. Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yanasema magaidi hao wa kigeni nchini Syria wametekeleza jinai za kivita.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO