Monday, June 17, 2013

MUSEVEN AUNGA MKONO HATUA YA ETHIOPIA

Huku hatua ya Ethiopia ya kujenga bwawa katika Blue Nile ikiendelea kuzidisha mivutano kati ya nchi hiyo na Misri, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameunga mkono ujenzi huo. Kwa mujibu wa toleo la leo la gazeti la  Wall Street Journal  la Marekani, Museveni ameounga mkono mradi huo wa Ethiopia na kwamba anaamini kuwa Addis Ababa na nchi nyinginezo za Kiafrika zinahitajia vituo vya kuzalisha umeme ili kuimarisha uchumi wao. Kwa mujibu wa gazeti hilo, gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni dola bilioni 4 na milioni 700 na kwamba Misri inapinga ujenzi huo kwa kuwa unapunguza fungu lake la maji katika Mto Nile.
Kutokana na mivutano hiyo Rais Muhammad Mursi wa Misri ametangaza kuwa ingawa Cairo haitaingia katika uwanja wa vita na Addis Ababa kwa sababu ya ujenzi huo lakini itatumia kila chaguo linalowezekana kuzuia ujenzi huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO