Sunday, June 16, 2013

SYRIA YAULAANI UAMUZI WA MISRI

Serikali ya Syria imeulaani uamuzi wa Misri wa kuuvunja uhusiano wake wa kibalozi na nchi hiyo na kuwaunga mkono waasi wanaopambana na utawala wa Rais Bashar al- Assad. Syria imeuita uamuzi huo kuwa ni hatua ya kutowajibika.
Afisa mmoja wa serikali ya Syria ambae hakutaka kutajwa jina ameliambia shirika la habari la serikali ya nchi yake,SANA kwamba Jamhuri ya Kiarabu ya Syria inaulaani uamuzi huo wa kutowajibika na amemlaumu Rais Mursi wa Misri kwa kijihusisha na njama dhidi ya Syria.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO