Sunday, June 16, 2013

BUNGE LAVUNJWA KUWAIT

Kuwait imesema mahakama ya katiba ya nchi hiyo imelivunja bunge baada ya sheria za uchaguzi kupingwa na hivyo kulazimisha kufanyika uchaguzi mpya unaoweza kuanzisha mivutano ya kisiasa na mapambano katika nchi hiyo ya Ghuba.
Uamuzi huo wa mahakama unafuatia kupingwa kwa sheria ya kupiga kura katika uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita, uliosusiwa na wapinzani na pande zingine zilizodai kwamba sheria mpya za uchaguzi zinaipendelea familia ya watawala, na kwamba sheria hizo zilipachikwa bila  ya mjadala wa wananchi. 
Shirika rasmi la habari la Kuwait limesema kwamba uamuzi wa mahakama unalibatilisha bunge la wajumbe 50.
Hata hivyo gazeti linaloegemea upande wa serikali,"Al Watan"limesema kuwa mahakama imeziacha kanuni za uchaguzi kama zilivyo, hali  inayosababisha wasi wasi juu ya kuendelea kwa mivutano ya kisiasa nchini Kuwait.
  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO