Friday, June 14, 2013

WAKIMBIZI WAREJEA KUTOKA UTURUKI

Idara Kuu inayojishughulisha na kupambana na matatizo ya kimaumbile na dharura ambayo ni taasisi ya Waziri Mkuu wa Uturuki, imetangza habari ya kurejea makwao wakimbizi wapatao laki moja na 24 elfu kutoka Syria. Ripoti iliyotangazwa leo na idara hiyo, imesema kuwa, tangu ulipoanza mgogoro wa Syria hadi sasa, wakimbizi wapatao laki moja na 24 elfu na 199 wa Syria, wamerejea nchi kwao kutoka Uturuki. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, hadi sasa bado kuna wakimbizi wapatao laki mbili na 91 katika vitongoji 14 vilivyoandaliwa kwa ajili ya kuwahifadhi wakimbizi hao katika mikoa ya mpakani ya Uturuki. Aidha Idara Kuu hiyo ya kukabiliana na matatizo ya kimaumbile na dharura imedai kuwa, mbali na idadi hiyo, kuna raia wengine laki mbili na 90 elfu wa Syria ambao wanaishi katika miji tofauti ya mpakani ya nchi hiyo na nje ya kambi hizo zilizotajwa. Hii ni katika hali ambayo, kufuatia kujiri mashambulizi ya kigaidi dhidi ya mji wa Reyhanli, raia wenye misimamo ya kufurutu mipaka wa Uturuki, wamewashambulia na kuwajeruhi wakimbizi kadhaa wa Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO