Wednesday, June 05, 2013

WAPALESTINA KUPIGANIA HAKI ZAO ICC NA ICJ

Saeb Uraiqat, kiongozi wa timu ya mazungumzo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametishia kuuburuza utawala wa Kizayuni wa Israel mbele ya vyombo vya sheria vya kimataifa iwapo Wapalestina hawatopata haki kupitia njia za kidiplomasia. Uraiqat amesema Israel imekuwa ikikwamisha mazungumzo kwa kukataa kutambua taifa huru la Palestina katika mipaka ya 1967. Amekumbusha kuwa, Palestina sasa ina haki kamili ya kuwasilisha kesi mbele ya mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC na vilevile mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ. Matamshi ya Uraiqat yametolewa huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry akitarajiwa wiki ijayo kuitembelea Israel pamoja na ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni katika kile kinachodaiwa kuwa ni juhudi za kufufua mazungumzo eti ya amani kati ya Palestina na Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO