Mashirika ya kijasusi ya utawala haramu wa Kizayuni, yameanza kutekeleza njama kabambe za kueneza utumiaji wa madawa ya kulevya kati ya vijana wa Kipalestina. Mashirika hayo ya kijasusi likiwemo shirika la kiintelijensia na usalama wa ndani wa Israel, kwa pamoja yanawatumia vibaraka kwa ajili ya kutekeleza mpango huo ikiwa ni pamoja na kusambaza mihadarati katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Wapalestina. Katika kuingiza madawa hayo ya kulevya, maafisa hao wa utawala haramu wa Kizayuni, wanawatumia Wapalestina ambao walikimbia Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina kwa tuhuma za kutenda jinai. Wengi wa watuhumiwa hao wanaotumiwa na Israel, walitiwa mbaroni na maafisa wa usalama huko Gaza. Wakati huo huo, askari haramu wa utawala huo bandia, wamewatia mbaroni Wapalestina 27 kutoka katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds. Hii ni katika hali ambayo duru za habari zimeripoti juu ya kuzorota hali ya mfungwa Abdullah Barghuthi, katika jela za kutisha za utawala huo. Wakili mtetezi wa mateka wa Palestina, ameelezea hali mbaya ya mfungwa huyo mwenye asili ya Jordan anayeshikiliwa katika korokoro za utawala huo katili wa Kizayuni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO