Saturday, July 06, 2013

KIONGOZI WA UPINZANI RUSSIA AHUKUMIWA KIFUNGO JELA

Alexei Navalny kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini Russia ambaye alitiwa mbaroni na jeshi la polisi kwenye maandamano hapo jana, huenda akatumikia kifungo cha miaka sita jela. Waendesha mashtaka nchini Russia wameitaka Mahakama ya Kirov nchini humo kumfunga Navalny kwa tuhuma za kufanya ubadhirifu mkubwa wa mali nchini humo. Iwapo hukumu hiyo itatolewa, itamfanya kiongozihuyo wa upinzani ashindwe kushiriki kwenye uchaguzi wa raia utakaofanyika mwaka 2018 nchini humo. Waendesha Mashtaka hao wa Russia wameitaka mahakama hiyo kumpiga faini ya dola elfu thelathini. Navalny anatuhumiwa kwa kulitia hasara dola laki tano kwenye bajeti iliyotengwa katika jimbo la Kirov wakati alipokuwa akihudumu kama Gavana wa  jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO