Saturday, July 06, 2013

MUGABE ATISHIA KUJITOA SADC

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametishia kujiondoa nchi yake kwenye uanachama wa Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC. Taarifa zinasema kuwa, tishio hilo la serikali ya Zimbabwe limetolewa baada ya kutolewa msisitizo wa jumuiya hiyo wa kufanyika marekebisho ya demokrasia kabla ya kufanyika uchaguzi ujao wa rais na bunge nchini humo. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara  uliohudhuriwa na wafuasi wa chama chake cha Zanu PF, Rais Mugabe amesema kuwa, maamuzi ya SADC siyo ya kimantiki, na kusisitiza kwamba Zimbabwe inaweza kujiondoa kwenye jumuiya hiyo.  Awali Rais Mugabe alitangaza kuwa, uchaguzi ujao ungelifanyika tarehe 31 Julai, lakini wapatanishi kutoka SADC walishinikiza uchaguzi huo usogezwe mbele kwa muda wa wiki mbili, ili yaweze kufanyika marekebisho ya kidemokrasia nchini humo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Godfrey Chidyausiku Jaji Mkuu wa Zimbabwe amesema kuwa, Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo haina mamlaka ya kubadilisha tarehe ya uchaguzi wa rais iliyotangazwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO