Friday, July 05, 2013

KOREA KUSINI YATAKA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KASKAZINI

Korea Kusini leo hii imependekeza mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu kulifunguwa upya eneo la viwanda la pamoja ambalo lilifungwa baada ya kuwepo kwa mvutano mkubwa wa kijeshi. Pendekezo hilo linakuja siku moja baada ya Korea Kaskazini kurudisha mawasiliano ya simu ya mpakani na kutangaza itawaruhusu wafanyabiashara wa Korea Kusini kuzuru eneo hilo la Kaesong lililoko hatua chache kutoka mpaka wa Korea Kaskazini ili kuvifanyia ukaguzi viwanda vyao vilivyofungwa.
Wizara ya Korea Kusini inayoshughulikia suala la Muungano wa Korea imetuma ujumbe kwa Korea Kaskazini kupendekeza mkutano katika kijiji cha mpakani cha suluhu cha Panmunjom hapo Jumamosi. Kimsingi Korea Kaskazini imekubali kufanyika kwa mkutano huo lakini imesisitiza ufanyike katika eneo la Kaesong. Mipango ya kuwa na mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu mustakbali wa eneo hilo lililofungwa tangu mwezi wa Aprili yalivunjika mwezi uliopita kutokana na mzozo wa itifaki.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO