Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imetoa taarifa kali inayokosoa misimamo ya kindumilakuwili ya Wamagharibi kuhusiana na matukio na hali ya mambo kwa ujumla nchini Syria. Taarifa hiyo imesisitiza kwamba, misimamo ya madola ya Magharibi kuhusiana na matukuo ya Syria haizingatii uhakika na uhalisia wa mambo. Russia imesisitiza kwamba, inasikitishwa mno na misimamo ya madola ya Magharibi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na kadhia ya Syria. Sehemu nyingine ya taarifa ya wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imebainisha kwamba, inasikitisha kuona kwamba, madola ya Magharibi yamekuwa yakitanguliza mbele maslahi yao ya kisiasa kuhusiana na kadhia ya Syria badala ya kuzingatia uhakika wa mambo ulivyo. Kwa mara nyingine tena Russia imesisitiza kwamba, kadhia ya Syria inapaswa kupatiwa ufumbuzi kwa njia za kidiplomasia na kisiasa na kwamba, nguvu za kijeshi sio utatuzi mwafaka wa mgogoro wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO