Friday, July 12, 2013

WANANCHI WABAHRAIN WAENDELEA NA MAANDAMANO

Maeneo tofauti nchini Bahran yameshuhudia maandamano ya usiku kulalamikia ukandamizaji na utesaji unaofanywa na polisi wa utawala wa ukoo wa kifalme wa Aal Khalifa dhidi ya wanawake na wanaume katika magereza ya utawala huo.
Maandamano hayo yamefanyika sambamba na kuendelea kuhukumiwa kinyemela idadi kubwa ya wanaharakati na watetezi wa haki za binaadamu nchini humo.
Hata hivyo maandamano hayo ya amani, yalikandamizwa na polisi waliotumia mabomu ya kutoa machozi na silaha nyinginezo.
Mahakama ya Bahran imeanza kuwahukumu watuhumiwa wa kesi inayofahamika kwa jina la 'Mtandao wa Februari 14' ambapo katika kikao cha kwanza, watuhumiwa wameelezea kuteswa sana na maafisa wa polisi ndani ya magereza ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO