Sunday, July 07, 2013

WATUNISIA WAANDAMANA KUPINGA UHUSIANO NA ISRAEL

Wananchi wa Tunisia wameandamana wakitaka kuhuishwa kipingee cha sheria  kuhusu 'kupigwa marufuku uhusiano na utawala wa Kizayui wa Israel' katika katiba ya nchi hiyo.
Katika maandamano yaliyofanyika Jumamosi nje ya jengo la bunge mjini Tunis, wananchi waliokuwa na hasira waliteketeza moto bendera za utawala wa Kizayuni na kutpiga nara za kuunga mkono mapambano ya Wapalestina wanaopigania ukombozi wa ardhi zao zilizotekwa na Israel.  Ahmad Al Kehlawi Mkuu wa Jumuiya ya Kuunga Mkono Mapambanno ya Wapalestina na Kupinga Uhusiano na Israel amesema rasimu ya tatu ya katiba mpya ya Tunisia haina kipengee cha kuharamisha uhusiano na Israel na kwamba jambo hilo linatia wasi wasi. Ameongeza kuwa katika rasimu ya kwanza ya katiba kulikuwa na kipengee kilichoutaja Uzayuni kuwa pote la ubaguzi wa rangi na kupinga uhusiano wowote ule na utawala wa Kizayuni wa Israel. Hata hivyo ameelezea masikitikio yake kuwa kufuatia mashinikizo ya kigeni kipengee hicho kimeondolewa katika rasimu mpya. Wanaharakati wa kijamii nchini Tunisia wamesema hawataruhusu mashinikizo ya kigeni yafanikishe njama za kuondoa kipengee hicho dhidi ya Israel katika katiba mpya ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO