Je, unahitaji kwenda kusoma nchini Turkey? Bado hujapitwa, wahi sasa kwani wakati ndio huu. Turkey ni miongoni mwa nchi zilizoendelea duniani inayopatikana kati ya bara la Europe na Asia. Mpaka sasa kuna wanafunzi wengi sana kutoka nchi mbalimbali duniani wanaosoma nchini humo ikiwemo watanzania wengi wanaopatikana katika miji mbali mbali ya nchi hiyo kama Istanbul, Ankara, Izmir na miji mingine. Kuna vyuo vingi sana vya kisasa, hivyo serikali ya Uturuki imetoa nafasi nyingi sana (scholarships) katika vyuo vilivyopo nchini humo kwa wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma huko katika fani mbali mbali. Vipo vyuo vinavyotoa mafunzo kwa kituruki na vingine kwa kingereza. Lakini moja ya masharti yao ni lazima usome kituruki ukiwa mwanafunzi nchini humo. Lugha hii sio ngumu pindi utakapoingia darasani na kuisoma. Wapo wanafunzi wengi kutoka nchi mbali mbali wamejifunza na wanaijua vizuri lugha hii. Miongoni mwa huduma utakazopewa ni pamoja na ada ya shule, ticket ya kwenda na kurudi kutokea nchini mwako , hostel na mengine mengi. Kumbuka kabla ya kuchagua chuo, hakikisha kinatambuliwa na TCU ili usije pata matatizo pindi utakapomaliza masomo yako na kurudi Tanzania. Pia maombi yote yafanyike mtandaoni kupitia website halali iliyoidhinishwa na wizara ya nchi hiyo ambayo ni www.turkiyeburslari.gov.tr. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19/05/2014. Unaweza kubofya hapa kutazama video ni jinsi gani ya kutuma maombi kwa urahisi. Kutokana na kuwa ni watu wengi duniani wanaofuatilia website hiyo inaweza kuwa inasumbua kufunguka kwa kipindi fulani, hivyo endelea kuifungua kila mara mpaka pale itakapokubali. Pia unaweza kufatilia taarifa zao za kila mara kupitia ukurasa wao wa Facebook hapa. KILA LA KHERI!!!!!