Thursday, June 26, 2014

AL-QAEDA WASHAMBULIA UWANJA WA NDEGE WA YEMEN

Muda mfupi uliopita inasemekana wanamgambo wa Al-Qaeda wamehusika na shambulizi la uwanja wa ndege wa Yemen. Shambulizi limeathiri mnara wa kuongozea ndege, haya yamesemwa na viongozi wa ulinzi katika uwanja huo. Walinzi hao wanasema shambulizi hilo katika uwanja wa ndege wa Sayoun uliopo katika jimbo la kusini la mji wa Hadramawt lilanza kutoka maeneo matatu tofauti mapema Alhamisi ya leo.
Kutokana na shirika la utangazaji la AFP wanataarifu kuwa mpaka sasa wanajeshi watatu wameshafariki kutokana na shambulizi hilo japokwa kituo cha utangazaji cha aljazeera hawajathibitisha habari hizo. Inasemekana shambulizi hilo limetokea saa chache baada ya walinzi kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi katika mji huo unaojulikana kuwa miongoni mwa ngome kuu za wanamgambo wa Al-Qaeda.  

Chanzo: Al-Jazeera


No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO