Sunday, December 02, 2012
MAREKANI YAKOSOLEWA KIMATAIFA KWA KUIUNGA MKON ISRAEL
Habari zinasema kuwa Marekani imeazimia kujenga kituo cha kijeshi cha chini ya ardhi kwa ajili ya utawala wa Kizayuni.
Gazeti la Washington Post limeandika kuwa timu ya wahandisi ya jeshi la Marekani imetangaza tenda ya makubaliano hayo ambapo kwa mujibu wake timu hiyo itajenga kituo cha kijeshi cha chini ya ardhi kitakachokuwa na ghorofa tano katika kituo cha jeshi la anga karibu na Tel Aviv. Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta ametangaza kuwa Washington itaendeleza misaada yake kwas Israel ili kuimarisha ngao za makombora ya utawala huo wa Kizayuni. Panetta amesema kuwa katika wiki chache zijazo Marekani inataraji kuipatia Israel mamilioni ya dola ili kuimarisha mfumo wake wa kujikinga na makombora.
Kuendelezwa uungaji mkono wa pande zote wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umekuwa na nafasi muhimu katika jinai za utawala huo kumekabiliwa na malalamiko na ukosoaji mkubwa kimataifa. Gazeti la The Guardian linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa kundi la washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na idadi kadhaa ya wasanii maarufu na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wametaka utawala wa Kizayuni uwekewe vikwazo vya kimataifa kutokana na mashambulizi yake ya kinyama ya hivi karibuni katika vita vya siku nane dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza.
Mairead Maguire, Nelson Mandela na Adolfo Perez Esquivel ni miongoni mwa wanaharakati watetezi wa amani na shakhsia wa kitamaduni na kisanaa waliosaini barua inayokosoa ushirikiano wa Marekani, Utawala wa Kizayuni na Umoja wa Ulaya na wametoa wito wa kuwekewa vikwazo utawala haramu wa Israel.
Hakuna shaka kuwa uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa utawala wa Kizayuni wa Israel umechangia sana katika kuendeleza jinai na vita vya utawala huo dhidi ya Wapalestina kama vile vita vya siku nane vya hivi karibuni huko Ghaza. Misaada rasmi ya Marekani isiyo na masharti ya kila ya mwaka kwa utawala wa Kizayuni ni dola bilioni tatu huku duru za kisiasa na za habari zikisema kuwa, misaada hiyo ya Marekani ni mikubwa zaidi kuliko kiwango hicho kilichotajwa. Imeelezwa kuwa Marekani inaipatia pia Israel misaada ya kijeshi isiyo na masharti kwa visingizo mbalimbali ambayo huwa haitangazwi.
Hii ni pamoja na kuwa Marekani na vilevile nchi za Ulaya huupatia utawala haramu wa Israel fedha na silaha za mabilioni ya dola ambazo sehemu yake kubwa hutumiwa na Israel kwa ajili ya kununulia silaha kutoka Marekani na nchi za Ulaya.
Kuongezeka misaada ya kijeshi ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni kunajiri katika hali ambayo katika miezi ya hivi karibuni pande hizo mbili zilishadidisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwa ajili ya kuimarisha mashirikiano ya kijeshi ya madola hayo ya kibeberu. Katika fremu hiyo wiki kadhaa kabla ya kuanza vita vya siku nane vya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza, Marekani na utawala wa Kizayuni zilifanya mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo wachambuzi wa masuala ya kisiasa waliyatathmini kuwa ni ruhusu ya Washington kwa utawala wa Kizayuni ili kwa ajili ya vita vya Ghaza.
Hata hivyo kushindwa Marekani kufikia malengo yake huko Iraq na Afghanistan na pia kushindwa kwa fedheha utawala wa Kizayuni wa Israel hivi karibuni katika vita vya siku nane dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza ni dhihirisho tosha kuwa Washington na Tel Aviv haziwezi kufuadafu licha ya kumiliki silaha za kisasa na kushirikiana pakubwa kijeshi mbele ya irada za mataifa mengine.
IRAN KUTUMA CHAKULA CHA MSAADA MYANMAR
Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema itatuma shehena kubwa ya misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya Waislamu wanaodhulumiwa nchini Myanmar.
Mkuu wa masuala ya habari katika Hilali Nyekundu ya Iran Pouya Hajian amesema shehena hiyo ya kwanza ya misaada inajumuisha tani 15 za vyakula na tani 15 za bidhaa nyingine za dharura.
Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wamekuwa wakikandamziwa na kuteswa katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia inayotawaliwa na Mabuddha. Katika miezi ya hivi karibuni Mabuddha wenye misimamo mikali wamekuwa wakiwashambulia Waislamu na kuteketeza moto misikiti na nyumba zao.
Maelfu ya Waislamu wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao katika hujuma zinazotekelezwa na Mabudhha. Umoja wa Mataifa unasema Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar ndio jamii inayokandamizwa zaidi duniani.
M23 WASHAMALIZA KUHAMA TOKA GOMA
Waasi wa M23 wameondoka kikamilifu katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Waasi hao ambao inadaiwa wanapata himaya ya Rwanda na Uganda waliuteka mji huo tarehe 20 mwezi uliopita wa Novemba. Goma ni mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini na mji huo unakadiriwa kuwa na wakaazi milioni moja. Siku ya Jumamosi wapiganaji 300 walionekana wakiondoka Goma wakiwa katika msafara wa magari waliyopora. Siku ya Ijumaa waasi hao pia waliondoka katika mji wa Sake ulio kilomita 30 magharibi mwa Goma. Brigedia Jeffrey Muheesi wa Uganda ambaye yuko katika ujumbe wa Nchi za Maziwa Makuu unaosimamia zoezi la kuondoka waasi hao Goma amesema wapiganaji wote wa M23 wameondoka mjini humo.
Kamanda wa M23 Brigedia Jenerali Sultani Makenga amesema wanataka serikali ya Kinshasa ianzishe mazungumzo katika muda wa masaa 48 na ameonya kuwa wanaweza kurudi tena Goma kwa mtutu wa bunduki iwapo mazungumzo yatafeli.
MAHASIMU WA AL-SHABAB WAJIUNGA NA SERIKALI YA SOMALIA
Wanamgambo wa Ahlu Sunnah Wal Jama’a wamejiunga rasmi na serikali ya Somalia na baada ya kupigana kwa muda wa miaka miwili bega kwa bega na vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Al Shabab.
Akizungumza Jumamosi mjini Mogadishu, kamanda wa ngazi za juu wa wanamgambo wa Ahlu Sunnah Sheikh Mohamed Yusuf Hefow amesema kuwa wapiganaji wa kundi lake sasa wameingia katika jeshi la serikali ya Somalia.Ahlu Sunnah Wal Jama’a Somalia wanakadiriwa kuwa na wapiganaji 2000 na aghalabu ni wafuasi wa itikadi ya Kisufi. Wamekuwa wakipigana dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab tokea mwaka 2008 baada ya wafuasi wa Al Shabab kuhujumu maeneo ya Masufi katika eneo la Galgaduud kati mwa Somalia.
MURSI ATANGAZA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA
Rais Mohammad Morsi wa Misri ametangaza kuwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo itafanyika Desemba 15 mwaka huu wa 2012.
Akizungumza Jumamosi mjini Cairo wakati akipokea rasmi nakala ya rasimu ya katiba mpya, Morsi aliwahakikishia watu wa Misri kuwa atatekeleza majukumu yake kwa maslahi ya taifa.
Mapema jana, kote Misri kulifanyika maandamano ya makumi ya maelfu ya watu wanaomuunga mkono rais Morsi pamoja na rasimu mpya ya katiba inayosema nchi hiyo itaongozwa kwa msingi wa sheria za Kiislamu.
Siku ya Ijumaa wapinzani wa Morsi waliandamana mjini Cairo wakipinga katiba mpya na uamuzi wa Morsi kujiongezea madaraka.
Rais wa Misri amesema hatua yake ya kujiongezea madaraka ni ya muda mfupi tu kwa lengo la kulinda mapinduzi ya wananchi. Ameongeza kuwa katiba mpya ikipitishwa madaraka ya rais yatapungua kwa kiasi kikubwa.
BEIT EL AJAB LAPOROMOKA
Aibu iliyoje leo kufikia Beit-el-Ajaib kuanguka baada ya Serikali kupuuza hatua zote za kuwazindua kuwa jengo hilo liko katika hali mbaya. Katika kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi cha mwezi Juni/Julai 2011 na 2012 nilizungumzia suala la uwezekano wa majengo haya ya kihistoria kuanguka kutokana na kutotunzwa au kufanyiwa matengenezo. Nikaandika na swali maalum kuhoji matengenezo ya majengo hayo hasa baada ya mradi wa MACEMP unaofadhiliwa na nchi wahisani na mashirika ya kimataifa kuwa na fungu la matengenezo la majengo ya Kasri (Palace) na Beit-el-Ajaib.
Kama kawaida ya majibu ya Serikali, tuliambiwa, ‘Tusiwe na wasiwasi’. Nikatahadharisha kuwa binafsi nimeyatembelea majengo hayo mawili kuona pamefanyika matengenezo gani kutokana na fedha zilizotengwa, na kuona hapana matengenezo ya maana. Nikajibiwa, ‘Tutafuatilia’. Sasa leo hii turathi ya kitaifa (national heritage) ambayo ni jengo la kwanza refu katika Afrika Mashariki, la kwanza kuwa na umeme na la kwanza kuwa na lifti kiasi cha kuitwa Jumba la Ajabu (House of Wonders) limeanguka kwa uzembe wa Serikali.
Saturday, December 01, 2012
NORTH KOREA YATOA TAARIFA YA URUSHAJI ROCKET
Pyongyang, North Korea- yatoa taarifa juu ya
urushaji wake wa Long-Range Rocket katikati ya mwezi huu ambayo inakiuka
matakwa ya Umoja wa Mataifa juu ya mipango yake ya nyuklia na makombora. Tukio hilo
linategemewa kufanyika mnazo tarehe 10 hadi 22, na litakuwa la pili chini ya
utawala wa kiongozi mpya wa taifa hilo Kim Jong Un ambaye aliingia madarakani
baada ya kufariki baba yake Kim Jong Il.
Msemaji wa kamati ya masuala ya anga amesema
kuwa wamegundua tatizo lililoifanya ifeli mara ya kwanza mwezi April mwaka huu.
Uzinduzi huo kwa niaba ya Kim Jong Il ambaye desemba 17,2011 alifariki na
kutarajia kuwa hiyo itakuwa ni ukumbusho wake.
Wakati huohuo marekani imesema majaribiao hayo
ni njia ya Korea kujaribu makombora yake ya masafa marefu zaidi ambayo
yanatarajiwa kuifikia marekani.
DEMOKRASIA YANAWIRI SOMALILAND
Uchaguzi wa mitaa unafanyika katika Jamhuri iliyojitangazia uhuru wake ya Somaliland , ambayo ilijitenga na Somalia zaidi ya mika ishirini iliyopita .
Uchaguzi huo haufanyiki katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo ambayo yana mzozo na jimbo jirani la Puntland.
Inaripotiwa kuwa watu wengi wamejitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo na kuna misururu mirefu nje ya vituo vya kupigia kura
Tangu ilipojitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991, Somaliland imekuwa ikipata mafanikio taratibu , lakini thabiti kuelekea demokrasia.
Hadi uchaguzi huu, ni vyama vitatu vilivyo ruhusiwa kuendesha shughuli zake . Sasa mfumo umewekwa na vyama saba vinachuana katika uchaguzi wa mitaa .
Vitatu vitakavyopata kura nyingi zaidi katika maeneo yote ya Somaliland vitaendelea kushindana katika uchaguzi wa bunge . Somaliland ni moja ya maeneo machache ya Somalia yaliyo na amani yanayoweza kuendesha uchaguzi .
Huenda maeneo mengine mengi ya Somalia yakasubiri kwa miaka kadhaa kabla ya kuweza kutekeleza haki yao ya kupiga kura.
Taarifa zinazohusiana
IRAN KARIBU ITAKUWA NA MFUMO WA KUZUIZ MAKOMBORA
Waziri wa Ulinzi wa Iran,
Ahmed Vahidi amesema kuwa nchi hii inaendelea vyema na mpango wake wa kuuda
mfumo wa kukabiliana na makombora unaoshabihiana na ule wa S-300 wa Russia.
Vahidi amesema wataalamu wa humu nchini wanakaribia kukamilisha shughuli hiyo
na kwamba karibuni hivi nchi hii itastafidi na ngao hiyo dhidi ya makombora.
Waziri wa Ulinzi amesisitiza kuwa, mfumo huo utakuwa na nguvu kushinda Kuba la
Chuma (Iron Dome) ya utawala haramu wa Israel. Juhudi za Iran za kujitengenezea
ngao dhidi ya makombora zimeimarika zaidi baada ya Russia kukataa kuiuzia ngao
ya S-300 licha ya pande mbili kutiliana saini makubaliano ya mauziano hayo
mwaka 2007
RAIS WA TUNISIA ATAKA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI
Rais Munsif Marzouki wa Tunisia amemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hamadi Jebali kuteuwa baraza jipya la mawaziri huku wananchi wakiendelea kuandamana wakilalamikia hali ngumu ya maisha nchini humo. Rais wa Tunisia amesema serikali ya mseto ya nchi hiyo imeshindwa kukidhi matakwa ya wananchi na kutaka kuundwa serikali mpya ndogo itakayoweza kushughulia hali ya machafuko iliyoikumba nchi hiyo sasa. Munsif Marzouki amesema chaguzi mpya zinapasa kufanyika haraka iwezekanavyo nchini humo kabla ya msimu ujao wa joto na kuitaja hali ya machafuko iliyoigubika nchi hiyo kuwa jambo lisilokubalika. Amesema serikali ya nchi hiyo ni lazima ibadilishwe ili kupatikana serikali mpya ya wataalamu na si ile inayowajumuisha wanasiasa kutoka mirengo mbalimbali.
BRAHIMI ASISITIZA UINGIALIAJI WA KIJESHI NCHINI SYRIA
Lakhdar Brahimi Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Syria ametaka uwepo uingiliaji wa kijeshi nchini humo ili kukabiliana na hali mbaya inayoendelea kushuhudiwa nchini humo. Akizungumza mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Brahimi ameongeza kuwa, mapigano yamezidi kusambaa karibu nchi nzima ya Syria, hivyo kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuzuia maafa zaidi nchini humo. Amesema kuwa, waasi wa Syria wanasisitiza juu ya kung'atuka Rais Bashar Assad na washirika wake kabla ya kuanza mazungumzo yenye lengo la kutafuta njia za kuutatua mgogoro huo. Brahimi amesisitiza kuwa, mgogoro wa Syria ulipaswa utatuliwe kwa njia za mazungumzo, lakini hakuna matumaini ya kupatikana amani kwa njia hiyo. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Syria amesema kuwa, kuna ulazima wa kutumwa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo kitakachokuwa na uwezo mkubwa wa kuleta amani nchini humo.
NATO YAASISSI KITUO KIPYA CHA KIJESHI UTURUKI
Muungano wa kijeshi wa Nato umeasisi kituo kipya cha kijeshi katika mkoa wa Izmir magharibi mwa Uturuki huku muungano huo wa kujihami wa Magharibi ukiwa na mpango wa kuweka ngao ya kisasa ya makombora ya Patriot katika mpaka kati ya Uturuki na Syria. James Stavridis kamanda mkuu wa Nato amesema katika sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha kijeshi kuwa Nato imekuwa ikiiamini Uturuki tangu nchi hiyo iwe mwanachama. Akizungumza kuhusu kuwekwa ngao ya makombora ya Patriot huko kusini mwa Uturuki, kamanda wa Jeshi la Ardhini la Muungano wa Nato Jenerali Frederick Ben Hodges amedai kuwa hatua hiyo haina lengo la kuanzisha eneo lisiloruhusiwa kuruka ndege au mashambulizi.
AJALI YA NDEGE KONGO BRAZZAVILLE YAUWA 20
Watu wasiopungua 20 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya ndege ya mizigo kuanguka karibu na uwanja wa ndege huko Brazzaville mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo. Ndege hiyo aina ya Ilyushin-76 iliyotengenezwa katika Umoja wa Kisovieti ilianguka jioni ya jana saa 11 na nusu kwa wakati wa Brazzaville. Ndege hiyo ilikuwa ikitoka huko Pointe Noire mji wa pili kwa ukubwa huko Jamhuri ya Kongo na ilijaribukutua wakati mvua kubwa zikinyesha.
Watu waliofariki dunia ni pamoja na wakazi waliokuwa wakiishi katika eneo hilo ndege ilipoangukia huko Makazou katika mji mkuu Brazzaville. Mabaki ya ndege hiyo ya mizigo yameonekana yakiwa yametawanyika katika eneo kubwa. Wafanyakazi wa huduma za uokoaji wamefanikiwa kuutambua mwili wa rubani wa ndege hiyo aliyekuwa raia wa Ukraine.
Subscribe to:
Posts (Atom)








