Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametishia kuiangamiza kabisa Korea Kusini wakati nchi hiyo ikikabiliwa na vikwazo vipya vya kiuchumi na kidiplomasia kutoka Marekani na Umoja wa Mataifa kwa tuhuma za ukiukaji wa haki.Wasiwasi wa kijeshi katika rasi hiyo ya Korea umeongezeka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miaka kadhaa huku serikali ya Kikumunisti ya Korea Kaskazini chini ya Kim Jong Un ikitishia kuanzisha vita vya Kinuklia kulipiza kisasi vikwazo iliyowekewa na Umoja wa Mataifa baada ya kufanya jaribio lake la tatu la silaha za Atomiki mwezi uliopita.Aidha nchi hiyo imechukua hatua ya kivyake ya kutangaza kuyafutilia mbali makubaliano ya miaka 60 ya amani na Korea Kusini kama hatua ya kupinga mpango wa wa pamoja wa mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini ulioanza Jumatatu.Hata hivyo kitisho cha hivi karibuni cha kukiangamiza kisiwa cha Baengyeong,cha Korea Kusini kilicho na wakaazi 5000 kimeonekana kuwa na uzito hali inayozusha wasiwasi mkubwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO