Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Syria inakabiliwa na vita vya kila upande na vya kimataifa. Sheikh Naim Qassim amebainisha kwamba, kwa sasa Syria inakabiliwa na njama za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu. Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwamba, lengo la njama hizo ni kuuangusha mfumo unaotawala nchini Syria. Aidha Sheikh Naim Qassim amesisitza kwamba, njama dhidi ya Syria zinatokana na kuwa, nchi hiyo daima kuunga mkono muqawama na kuwa dhidi ya matakwa ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel sambamba na kuwa mstari wa mbele kuunga mkono kadhia ya Palestina. Sheikh Naim Qassim ameashiria chokochoko mpya tarajiwa za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mashariki ya Kati na kusema, endapo kutatokea kitu kama hicho Hizbullah ina haki kamili ya kujibu chokochoko na uvamizi huo wa Wazayuni.
Na Salum Bendera
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO