Wednesday, March 13, 2013
RUSSIA YATUMA MSAADA WA KIBINADAMU SYRIA
Russia imetuma shehena ya misaada ya kibinadamu nchini Syria ili kuwasaidia raia walioathiriwa na machafuko nchini humo. Ndege ya Russia jana ilitua katika uwanja wa ndege wa Bassel al Assad katika mkoa wa pwani wa Latakia ikiwa imebeba tani kumi za bidhaa za chakula na mablanketi. Mwanadiplomasia mmoja wa Russia amesema shehena hiyo ni msaada wa tano wa kibinadamu kutumwa na Russia huko Syria hadi sasa. Mwezi Oktoba mwaka jana pia Russia ilituma meli yenye misaada ya kibinadamu huko Syria, ambapo mingi kati ya hiyo ilikuwa ya madawa kwa ajili ya raia wa Syria. Russia na China zimepinga hatua ya nchi za Magharibi ya kutaka kuweka vikwazo ili kuishinikiza serikali ya Damascus.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO